MISRI

Thelathini na mbili wafariki dunia baada ya treni mbili kugongana Misri

Watu wakishiriki katika shughuli za uokoaji kuwa ondoa watu katika mabehewa baada ya treni mbili kugongana karibu na mji wa Sohag, Misri, Machi 26, 2021.
Watu wakishiriki katika shughuli za uokoaji kuwa ondoa watu katika mabehewa baada ya treni mbili kugongana karibu na mji wa Sohag, Misri, Machi 26, 2021. REUTERS - STRINGER

Takriban watu thelathini na wawili wamefariki dunia na wengine 66 wamejeruhiwa katika ajali ya treni mbili zilizogongana kaskazini mwa mji wa Sohag nchini, Misri katikati mwa nchi, leo Ijumaa, runinga ya Nile TV imeripoti, ikinukuu wizara ya afya.

Matangazo ya kibiashara

"Treni hizo mbili ziligongana (...) hali iliyosababisha mabehewa mawili kuharibika vibaya wakati la bewa la tatu lilipinduka," chanzo cha usalama kimeliambia shirika la habari la REUTERS.

Shirika la reli nchini Misri ni moja ya mashirika kongwe na lenye shughuli nyingi zaidi katika eneo hilo, na ajali hutokea mara nyingi kwenye njia zake.