COTE D'IVOIRE

Cote d'Ivoire: Kesi ya mashambulizi ya Bouaké kufunguliwa Paris

Askari wa Ufaransa mbele ya moja ya ndege mbili aina ya Sukhoi-25 ambazo zilitumika katika mashambulizi ya kambi ya Bouaké Novemba 6, 2004.
Askari wa Ufaransa mbele ya moja ya ndege mbili aina ya Sukhoi-25 ambazo zilitumika katika mashambulizi ya kambi ya Bouaké Novemba 6, 2004. AFP/Pascal Guyot

Mnamo Novemba 6, 2004, ndege mbili za Cote d'Ivoire zilishambulia kambi ya wanajeshi wa Ufaransa kutoka kikosi cha Licorne katika mji wa Bouaké, nchini Côte d'Ivoire: wanajeshi tisa wa Ufaransa na raia mmoja wa Marekani waliuawa, huku watu 38 wakijeruhiwa.

Matangazo ya kibiashara

Kwa kulipiza kisasi, jeshi la Ufaransa lilitekeleza mashambulizi dhidi ya kambi kubwa ya kijeshi ya kikosi cha wanaanga cha Cote d'Ivoire. Baada ya hapo kulifuatia mvutano mkali kati ya Paris na Abidjan.

Zaidi ya miaka 16 baadaye, kesi ya marubani walioshtakiwa kwa mauaji, jaribio la mauaji na uharibifu wa mali inafunguliwa leo Jumatatu mbele ya mahakama ya Paris, bila kuwepo washtakiwa.

Washtakiwa hawatakuepo katika kesi hiyo. Kati ya watuhumiwa watatu, mamluki wa zamani kutoka Belarusi Yury Sushkin, anayeshukiwa kuendesha moja ya ndege zilizotekeleza mashambulizi hayo, alitoweka. Marubani wenzake wawili wanaoshukiwa kuwa raia wa Cote d'Ivoire, Ange Magloire Gnanduillet Attualy na Patrice Ouei walisamehewa nchini mwao kutokana na sheria inayotoa msamaha ya mwaka 2007.

Hali ni "ngumu sana" ameelezea Edwige Laliche, ambaye alimpoteza mwanawe katika mashambulizi hayo. "Je! Unaweza kufikiria, wanamuua mtoto wako  na unawajua wauaji na unasikia wako huru!" Wamenikosesha mengi, wanayaweka maisha yangu hatarini, wameharibu vitu vingi. Kesi ipo, zaidi ya miaka kumi na sita baadaye, bado wako zao huru! Labda hapo ndipo pagumu zaidi, ”ameongeza.