DRC

Mazungumzo ya amani na usalama Kivu Kusini yaanza Kinshasa

DRC, Oktoba 2020: kati ya Minembwe na Mikenge, nyumba zilichomwa moto. Makumi ya maelfu ya watu katika nyanda za juu wamelazimishwa kuyatoroka makaazi yao kwa mwaka mmoja na nusu.
DRC, Oktoba 2020: kati ya Minembwe na Mikenge, nyumba zilichomwa moto. Makumi ya maelfu ya watu katika nyanda za juu wamelazimishwa kuyatoroka makaazi yao kwa mwaka mmoja na nusu. RFI/Sonia Rolley

Mazungumzo kati ya jamii kuhusu amani na usalama katika maeneo ya Fizi, Uvira na Mwenga (Itombwe) katika mkoa wa Kivu Kusini yameanza leo Jumatatu Machi 29, 2021 katika mji mkuu wa DRC, Kinshasa.

Matangazo ya kibiashara

Kwa muda wa siku 3, washiriki 150 watajadili namna ya kudumisha amani katika jamii za Wabembe, Babuyi, Wafuliru, Banyamulenge, Banyindu, Warundi na Bavira.

Kwa upande wa shirika la Interpeace, ambalo linaandaa mkutano huu, kwa ushirikiano na Wizara ya Mambo ya Ndani, linasela lengo ni kupata maazimio ambayo yanaweza kumaliza migogoro katika jamii hizi.

"Lengo kuu ni kufikia kwenye hatua zenye maamuzi, ili kurejelea upya mkataba uliokuwepo hapo zamani. Jamii kutoka maeneo hayo hazijaanza kujadiliana leo. Mchakato huu umeanza na ulisitishwa tangu mwezi Septemba 2019, "amesema Pacifique Borauzima, mwakilishi wa shirika la Interpeace nchini DRC kulingana na Redio Okapi inayodhaminiwa na Umoja wa Mataifa.

Amebaini kwamba amepewa jukumu la kuzindua tena mchakato huu wa mazungumzo, kisha kuifanya iwe endelevu na uongozi wa serikali ili "kuhakikisha kuwa maafikiano yaliyojadiliwa katika mazungumzo kati ya jamii huko Kinshasa yanaweza kuchangia na kutumika kama misingi ya programu katika serikali . "

Kulingana na Pacifique Borauzima, mafanikio ya mazungumzo haya kati ya jamii yanahitaji maamuzi yaliyofikiwa kati ya jamii kwa upande mmoja, lakini pia kati ya jamii na serikali kwa upande mwingine.

"Tutegemee kwamba kitendo hiki cha kujitolea kinaweza kutengenezwa kwa njia ya mpango wa amani, upatanisho na mshikamano wa kijamii katika maeneo hayo na mambo ambayo yanaonyesha mahitaji na sababu za msingi za mizozo na ukosefu wa usalama", amesema.