COTE D'IVOIRE

Wanajeshi watatu wauawa kaskazini mwa Cote d'Ivoire

Wanajeshi wa Cote d'Ivoire waliojeruhiwa huko Kafolo wasafirishwa Abidjan, Juni 11, 2020.
Wanajeshi wa Cote d'Ivoire waliojeruhiwa huko Kafolo wasafirishwa Abidjan, Juni 11, 2020. RFI/Pierre Pinto

Wanajeshi watatu wameuawa na wengine saba wamejeruhiwa leo Jumatatu asubuhi katika shambulio dhidi ya vituo viwili vya jeshi kaskazini mwa Côte d'Ivoire, vyanzo vitano vya jeshi vimebaini.

Matangazo ya kibiashara

Washambuliaji wawili wamepigwa risasi na kuuawa na wengine wanne walikamatwa, vyanzo hivyo vimeongeza

Hata hivyo hakua kudi ambalo limedai kuhusika a shambulio hilo.

Chanzo kimoja kimesema kuwa washambuliaji walitokea nchi jirani ya Burkina Faso, taarifa ambayo haikuweza kuthibitishwa.

Kulingana na vyanzo hivi vya jeshi, wanajeshi wawili wameuawa katika shambulio dhidi ya kambi ya kijeshi ya Kafolo, karibu na mpaka na Burkina Faso na kami amayo ililengwa na shambulio lillilogharimu maisha ya wanajeshi kumi na tatu wa Cote d'Ivoire  mnamo mwezi Juni 2020.