MALI

Uchunguzi UN: Mashambulizi ya anga ya Ufaransa yaliua raia 19 Mali

Msafara wa magari ya wanajeshi wa Ufaransa ukitikea Tombouctou ukielekea Gao.
Msafara wa magari ya wanajeshi wa Ufaransa ukitikea Tombouctou ukielekea Gao. REUTERS/David Lewis

Uchunguzi wa Umoja wa Mataifa unabaini kuwa mashambulizi ya anga ya jeshi la Ufaransa nchini Mali mnamo mwezi Januari yaliua raia 19 waliokusanyika kwa harusi, sio tu wanajihadi,kama ilivyo inavyoeleza Paris, kulingana na ripoti ambayo shirika la habari la AFP limepata kopi

Matangazo ya kibiashara

Mwishoni mwa uchunguzi uliofanywa na kitengo cha Haki za Binadamu cha tume ya Umoja wa Mataifa nchini Mali (Minusma), ukiungwa mkono na polisi wa uchunguzi wa Umoja wa Mataifa, katika matukio yaliyotokea Januari 3 karibu na mji wa Bounti (katikati mwa Mali), Minusma "imethibitisha kuwa kulikuwa na sherehe ya harusi ambayo iliyowakusanya raia zaidi ya mia moja, ikiwa ni pamoja na watu watano wenye silaha, wanaodaiwa kuwa wananamgambo wa kundi la wanajihadi la Katiba Serma ", muhtasari wa ripoti hiyo umethibitisha.

UN "yataka" kufunguliwa kwa uchunguzi

Kkundi la Katiba Serma lina uhusiano na kundi linalodai kutetea Uislamu na Waislamu (GSIM, au JNIM kwa Kiarabu), muungano wa makundi ya kijihadi unaofungamana na Al-Qaeda. Takriban watu 22 waliuawa, wakiwemo watu watatu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa kunfi la Katiba Serma - 19 papo hapo, 3 wakati wa likuwa wakisafirisgwa hospiotalini, ripoti hiyo ya uchunguzi imebaini.

Kundi lililoathiriwa "lilikuwa na idadi kubwa ya raia ambao ni watu wanaotakiwa kulindwa dhidi ya mashambulio chini ya sheria za kimataifa za kibinadamu," imesema Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Mali (Minusma).

Minusma "inapendekeza" kwa mamlaka ya Mali na Ufaransa kuanzisha "uchunguzi huru, wa kuaminika na wa uwazi".