COTE D'IVOIRE

ICC kuamua juu ya hatma ya Laurent Gbagbo

Laurent Gbagbo akiwasalimu wafuasi wake wake Februari 6, 2020 huko Hague.
Laurent Gbagbo akiwasalimu wafuasi wake wake Februari 6, 2020 huko Hague. AP - Jerry Lampen

Kesi ya rais wa zamani wa Cote d'Ivoire na waziri wake wa zamani Charles Blé Goudé ilianza mwezi Januari 2016. Wote wawili waliachiliwa huru katika kitengoch kwanza cha mahakama hiyo, mwanzoni mwa mwaka 2019, baada ya kushtumiwa uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita, katika muktadha wa vurugu zilizofanywa kati ya Desemba 2010 na Aprili 2011, kufuatia kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa urais. ICC inatarajia kutoa uamuzi juu ya kuachiliwa kwao huru leo Jumatano.

Matangazo ya kibiashara

Moja ya mambo muhimu ya kwanza ya kesi hii  ni kuingilia kati kwa timu ya Fatou Bensouda. Ofisi ya mwendesha mashtaka itawasilisha nyaraka kadhaa na imewaita mashahidi karibu 80 kuja kutoa ushuhuda, ikiwa ni pamoja na maafisa wa jeshi na kisiasa.

 

Lengo lake ni kuonyesha kuwa Laurent Gbagbo na Charles Blé Goudé walikuwa katika "kundi dogo", ambalo lilianzisha "mpango wa pamoja" wa kusalia madarakani, siku iliyofuata baada ya matokeo ya uchaguzi yaliyopingwa mwishoni mwa mwaka 2010.

"Ushahidi unaonyesha kuwa Laurent Gbagbo alikuwa akipokea habari juu ya maandalizi na uendeshaji wa mashambulio, na kwamba alikuwa akitoa maagizo," amesema Eric MacDonald, naibu mwendesha mashtaka mwandamizi. Sio muhimu kuonyesha kwamba mpango wa pamoja umeanzishwa kama vile mnavyojua: mpango wa pamoja hauwezi kuandikwa, au kuwekwa wazi. Lakini unaweza kutekelezwa kwa vitendo. Tasnifu yetu ni kwamba Laurent Gbagbo alikuwa ametoa maagizo ambayo yalisababisha kutekelezwa kwa uhalifu. Kwa mfano, mnamo Desemba 15, 2010, alituma wanajeshi dhidi ya wapinzani wa kisiasa walioandamana katika barabara za mjini Abidjan, Bwana Gbagbo alijua kuwa uhalifu utatokea ".

Gbagbo na Blé Goudé waachiliwa huru katika kitengo cha mwanzo cha ICC

Baada ya kusikilizwa kwa miaka miwili, kesi hiyo ilitatuliwa, majaji hawakukubaliana na mashtaka ya ofisi ya mwendesha mashtaka na kuruhusu upande wa utetezi wa Laurent Gbagbo na Charles Blé Goudé kuomba waanchiliwe huru, bila mashahidi wao kuletwa.