SOMALIA

Somalia: Uchaguzi wakwama, UN yatiwa wasiwasi

Wafuasi wa wagombea wa upinzani wanaandamana katika mji wa Mogadishu Februari 19, 2021.
Wafuasi wa wagombea wa upinzani wanaandamana katika mji wa Mogadishu Februari 19, 2021. AFP - -

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeelezea wasiwasi wake juu ya mgogoro wa kisiasa nchini Somalia kuhusu kufanyika kwa uchaguzi mpya, mkuu wa sera ya Marekani katika Umoja wa Mataifa.

Matangazo ya kibiashara

Muhula wa miaka minne wa Rais Mohamed Abdullahi Mohamed ulimalizika mwezi uliopita bila kuteuliwa mrithi wake. Bunge la Somalia lilitarajia kuchagua rais mpya Februari 8, lakini uchaguzi ulicheleweshwa kwani wabunge wapya hawajachaguliwa.

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield amesema wajumbe 15 wa Baraza la Usalama la Umoja wa Matifa "wamekaribisha juhudi zilizofanywa kupata makubaliano kati ya viongozi wa serikali ya shirikisho la Somalia na majimbo ya shirikisho" juu ya utekelezaji wa mfumo wa uchaguzi uliofanyiwa marekebisho.

"Wameelezea wasiwasi wao juu ya  mvutano wa kisiasa na wakatoa wito kwa viongozi wa Somalia kushiriki mazungumzo, bila masharti yoyote, ili kutatua maswala yaliyosalia," amesema.