DRC-RWANDA

Maswali yaibuka juu ya ushirikiano wa kijeshi kati ya DRC na Rwanda

Kikosi cha wanajeshi wa DRC (FARDC) wakikabiliana na waansi wa Uganda wa ADF.
Kikosi cha wanajeshi wa DRC (FARDC) wakikabiliana na waansi wa Uganda wa ADF. AFP

Jumanne hii, Machi 30, vikosi vya jeshi vya DRC (FARDC) vilitangaza kwamba watapanua ushirikiano wa kijeshi na majeshi ya nchi zilizo katika ukanda huo

Matangazo ya kibiashara

Mikutano ya pande mbili kati ya maafisa wa usalama wa DRC na wale wa Rwanda imeongezeka tangu Felix Tshisekedi awe madarakani. Lengo ni kukomesha makundi yenye silaha ambayo yamekita mizizi kwenye maeneo ya mipaka ya nchi hizo mbili. Taratibu za ushirikiano hazijawekwa wazi na hii inaibua maswali mengi kwa mashrika ya kiraia na viongozi waliochaguliwa.

FARDC inaelezea uamuzi huu kwa ulitokana na nia ya wakuu wa nchi za ukanda huo kukapambana dhidi ya ukosefu wa usalama, kikwazo kwa uimarishwaji wa uchumi wa nchi za ukanda. Kulingana na jeshi la DRC wajumbe mbalimbali kutoka nchi hizo wameanza kukutana. Wajumbe hao watafikia maendeleo ya mikakati kulingana na vyanzo vya kijeshi kutoka DRC.

Mpango wa pamoja

Hadi sasa, ni Rwanda na DRC tu ndio wameendelea sana juu ya suala hili. Katikati ya mwezi Machi, Mkuu wa majeshi ya Rwanda alipokelewa mjini Kinshasa. Mpango wa pamoja umetengenezwa. Walakini, hakuna habari iliyovuja kuhusina na mpango huo.

Kwa upande wa maafisa waliochaguliwa na mashirika ya kiraia, kuna hofu kwamba mpango huo utapelekea operesheni za pamoja za kijeshi mashariki mwa nchi ambapo tayari kunakabiliwa na ukosefu wa usalama.

Mwezi Desemba 2020, kundi la wataalam wa Umoja wa Mataifa katika DRC pia liliripoti kwamba operesheni za kijeshi zilitekelezwa na jeshi la Rwanda katika mkoa wa Kivu Kaskazini kati ya mwisho wa mwaka 2019 na mwanzo wa mwezi Oktoba 2020. Madai ambayo Kigali imekuwa ikikanusha kila wakati.

Swali lisilo na jibu

Hata hivyo katika kikao cha Bunge mnamo mwezi Januari, Mbunge Juvenal Munubo aliwahi kumuuliza Waziri wa Ulinzi swali juu ya uwepo wa jeshi la Rwanda kwenye ardhi ya DRC, lakini swali hilo halikujibiwa katika kikao hicho cha Bunge.