ETHIOPIA

Mataifa yenye nguvu za kiuchumi duniani yalaani dhulma dhidi ya raia Tigray

Wanajeshi wa Serikali ya Ethiopia, ambapo wanatuhumiwa kushambulia kiholela jimbo la Tigray
Wanajeshi wa Serikali ya Ethiopia, ambapo wanatuhumiwa kushambulia kiholela jimbo la Tigray EDUARDO SOTERAS AFP/File

Viongozi wa mataifa ya G7 yenye uchumi mkubwa duniani, wametaka kuondolewa kwa wanajeshi wa Eritrea katika jimbo la Tigray nchini Ethiopia, wakati huu Shirika la Kimataifa la utatatuzi wa mizozo, International Crisis Group likionya kuwa hali itaendelea kuwa mbaya katika eneo hilo.

Matangazo ya kibiashara

Katika hatua nyingine, picha mpya za video zilizochapishwa juma hili zinawaonesha wanajeshi wa Ethiopia wakitekeleza mauaji ya raia zaidi ya 30 kwenye jimbo la Tigray kwa kuwapiga risasi kutokea nyuma.

Viongozi kutoka mataifa yaliyostawi kiuchumi  (G7) wamesema "wana wasiwasi mkubwa" na ripoti za ukiukwaji wa haki za binadamu katika eneo lililokumbwa na mizozo nchni Ethiopia.

Eritrea imepuuzilia mbali madai hayo, wakati waziri mkuu wa Ethiopia hapo awali alikanusha taarifa za kuuawa kwa raia.