SOMALIA

Askari na waasi kadhaa wauawa kambi mashambulizi mawili Somalia

Somalia imeendelea kukumbwa na mashambulizi ya hapa na pale yanayotekelezwa na makundi yenye silaha.
Somalia imeendelea kukumbwa na mashambulizi ya hapa na pale yanayotekelezwa na makundi yenye silaha. © AFP - STRINGER

Kambi mbili za jeshi la Somalia zimeshambuliwa leo Jumamosi na wapiganaji wa kijihadi kutoka Al Shabaab,  kusini magharibi mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Mogadishu.

Matangazo ya kibiashara

Jeshi limeripoti majeruhi kutoka pande zote mbili na kusema limerejesha himaya yake katika kambi hizombili.

Wanajeshi "kadhaa" wameuawa katika shambulio hilo kwenye kambi za Bariire na Awdhigle, karibu kilomita 100 kutoka mji mkuu, amesema afisa mmoja wa jeshi. Washambuliaji kadhaa pia wameuawa, ameongeza.

"Tumekuwa tukiwatimua wanamgambo msituni," amesema msemaji wa jeshi.

Al Shabaab imesema imetekeleza mashambulizi yake kwenye kambi mbili ikitumia magari yaliyotegwa mabomu kuzuia jeshi kupeleka kikosi cha usaidi katika mj wa Bariire. Magari matatu ya kijeshi yameharibiwa, amesema Abdiasis Abu Musab, msemaji wa kundi hilila wanamgambo wa Kiismanu lenye mafungamano na Al Qaeda.