MALI-UN

Mauaji ya Dupont na Verlon: UN yashutumu Ufaransa kwa kukwamisha uchunguzi

Ghislaine Dupont na Claude Verlon.
Ghislaine Dupont na Claude Verlon. © ©RFI

Katika barua kwa mamlaka ya Ufaransa ambayo Magazeti ya Mediapart na "Guardian" vilipata kopi, mwandishi maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji ya kiholela, Agnès Callamard, anashutumu jeshi la Ufaransa kwa kuzuia uchunguzi wa Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji ya Ghislaine Dupont na Claude Verlon nchini Mali.

Matangazo ya kibiashara

Agnès Callamard pia ameshtumu mazingira ambayo amesema yameendelea kukwamisha uchunguzi wa Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji ya waandishi hao wa habari.

Katika barua yake ya kurasa 30 iliyotumwa kwa mamlaka ya Ufaransa na ambayo magazeti ya Mediapart na Guardian waliweza kupata kopi, Agnès Callamard hakufich kile anachosema kinazuia uchunguzi wa Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji hayo.

Miaka saba baada ya kuuawa kwa Ghislaine Dupont na Claude Verlon karibu na mji wa Kidal, mwandishi maalum wa Umoja wa Mataifa anasisitiza kwanza kwamba jeshi la Ufaransa linatumia vibaya sheria zihusuzo siri za taifa kuwazuia wachunguzi kupata ukweli. Agnès Callamard ameshutumu kuzuiwa kwa uchunguzi wa kimahakama na ukiukaji wa sheria za kimataifa.