NIGERIA

Nigeria: Zaidi ya wafungwa 1,800 watoroka jela

Nigeria yaendelea kukabilia na mdororo wa usalama.
Nigeria yaendelea kukabilia na mdororo wa usalama. AP - Francois Rihouay

Zaidi ya wafungwa 1,800 wametoroka jela baada ya shambulio la "watu wenye silaha dhidi ya jela hilo walilikokuwa wakizuiliwa, kusini mashariki mwa Nigeria", mamlaka ya magereza imesema.

Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo  dhidi ya jela hilo limrtokea leo Jumatatu (Aprili 5) katika jimbo la Imo, kusini mashariki mwa Nigeria

"Gereza la Owerri (...) limeshambuliwa saa 2:15 usiku, Jumatatu, Aprili 5, na watu wenye silaha wasiojulikana na kuwaachilia wafungwa 1,844," amesema Francis Enobore, msemaji wa mamlaka ya magereza katika taarifa, akibaini kwamba washambuliaji walitumia vilipuzi.