CAR

CAR: Kundi la UPC lajiondoa katika muungano wa waasi wa CPC

Kundi la waasi la UPC linaloongozwa na Ali Darassa limeaidi kujiondoa katika muungano wa wa waasi wa CPC.
Kundi la waasi la UPC linaloongozwa na Ali Darassa limeaidi kujiondoa katika muungano wa wa waasi wa CPC. AFP/File

Kundi la UPC, moja wapo ya makundi ya waasi yenye nguvu nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati, "limeamua" kujitoa katika muungano wa wa makundi ya waasi wa CPC. Hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumatatu jioni, taarifa ambayo imethibitishwa na msemaji wa kundi la waasi wa UPC.

Matangazo ya kibiashara

Muungano wa makundi ya waasi wa CPC, uliundwa mnamo mwezi Desemba mwaka jana na ambao tangu wakati huo lengo lake ni kumpindua Rais Touadéra.

Hati hiyo imeandikwa kwa mkono na kusainiwa na Ali Darassa. Kiongozi wa waasi ametangaza kwamba yeye na "maafisa wake" wameamua "kujiondoa katika muungano wa makundi ya waasi wa CPC", na " ameamua kujiunga [...] katika mchakato wa amani Khartoum".

Mkataba huu wa amani ulisainiwa mnamo mwezi Februari 2019 na makundi 14 yenye silaha, lakini ilishutumiwa mwezi Desemba na makundi sita kati ya makundi hayo ya waasi, ikiwa ni pamoja na kundi la waasila UPC, usiku wa kuamkia uchaguzi wa urais.