BURKINA FASO

Saba wauawa katika shambulizi la kushtukiza mashariki mwa Burkina Faso

Vikosi maalumu vya Burkina Faso vikiwa katika mafunzo.
Vikosi maalumu vya Burkina Faso vikiwa katika mafunzo. The Washington Post via Getty Im - The Washington Post

Angalau maafisa watatu wa polisi na wanamgambo wanne wanaoungwa mkono na mamlaka waliuawa Jumatatu wiki hi wakati walipokuwa wakipiga doria mashariki mwa Burkina Faso, kulingana na vyanzo kadhaa kutpka serikalini na vikosi vya usalama.

Matangazo ya kibiashara

Waathiriwa walivamiwa katika mji wa Tanwalbougou, katika mkoa wa Gourma, vyanzo vimesema, ambavyo havikutaka kutajwa majina yao, na kuongeza kuwa idadi ya waliouawa inaweza kuongezeka.

Raia hao wanne waliouawa walikuwa wanamgambo wa kundi la VDP, kundi linalofadhiliwa na ambalo liliundwa na serikali kupigana na waasi wa Kiisilamu.

Kufikia sasa hakuna kundi ambalo limedai kuhusika na shambulo hilo, lakini mashambulio ya waasi wanaohusishwa na Al Qaeda au Islamic State (IS) yamekuwa yakiripotiwa mara kwa mara nchini Burkina Faso na pia katika nchi jirani za Mali na Niger.