SUDAN

Sudan: Hali ya hatari yatangazwa Darfur Magharibi

Moja ya wakimbizi wa ndani katika kambi ya Al-Geneina, lmji mkuu wa jimbo la Darfour magharibi (picha ya kumbukumbu)
Moja ya wakimbizi wa ndani katika kambi ya Al-Geneina, lmji mkuu wa jimbo la Darfour magharibi (picha ya kumbukumbu) ASHRAF SHAZLY / AFP

Machafuko ya hivi punde kati ya makabila hasimu katika jimbo lenye mgogoro la Sudan yamesababisha vifo vya watu 50 na zaidi ya 120 wamejeruhiwa tangu Jumamosi, kulingana na chama cha Madaktari nchini Sudan.

Matangazo ya kibiashara

Mapigano haya yalianza Jumamosi huko El-Geneina, mji mkuu wa jimbo hili.

Matukio ya siku chache zilizopita yanatishia kuzidisha hali mbaya. Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa safari za ndege za kubeba misaada kwenda katika mji wa El-Geneina zimesitishwa. Hatua hii inaweza kuathiri zaidi ya watu 700,000.

“Tangu Aprili 3, watu 40 wameuawa katika mapigano ya hivi karibuni kati ya jamii ya Massalit na makabila ya Kiarabu. Hali inaendelea kuwa ya wasiwasi katika mji wa Al Geneina, ”Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na uratibu wa misaada ya kibinadamu (OCHA) ilisema katika taarifa ya hapo awali. "Tume ya misaada ya kibinadamu ya serikali inaripoti [...] watu 58 wamejeruhiwa," iliongeza OCHA.

Milio ya risasi ilisikika katika mji huo siku ya Jumatatu, huku watu wakionekena kutoroka makaazi yao wakihofia usalama wao.

Jimbo la Darfur tangu mwaka 2003 limekosa utulivu, mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, yamesababisha vifo vya watu zaidi ya Laki tatu na wengine Milioni 2.5 kuyakimbia makwao kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa.