CONGO BRAZZAVILLE

Ushindi wa Sassou Nguesso waidhinishwa

Rais wa Congo Brazzaville Sassou-Nguesso..
Rais wa Congo Brazzaville Sassou-Nguesso.. © AFP - Ludovic Marin

Mahakama ya Katiba ya Congo- Brazaville imeidhinisha Jumanne wiki hii ushindi wa rais Denis Sassou Nguesso wa Machi 21, baada ya upinzani kupinga ushindui huo na kuwasilisha malalamiko yake mbele ya Mahakama ya Katiba.

Matangazo ya kibiashara

"Katika matokeo ya mwisho ya uchaguzi (...), Mahakama ya Katiba imefanya marekebisho muhimu. Mgombea urais Denis Sassou Nguesso anatangazwa mshindi baada ya kupata 88.40% ya kura ”, ameitangaza Auguste Iloki, rais wa mahakama  ya juu zaidi nchini.

Wapinzani wa rais Nguesso walikataa kukubali matokeo hayo wakisema uchaguzi huo ulikumbwa na udanganyifu mkubwa.

Bwana Sassou-Nguesso alishinda kuidhinishwa kwa mabadiliko ya katiba mwaka jana ili kumruhusu agombee tena kwa muhula mwingine wa miaka 7 zaidi mamlakani.