MISRI

Ethiopia yatishia kutumia njia zingine katika mgogoro wa matumizi ya mto Nile

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sissi wakati wa ziara yake nchini Sudan Machi 6, 2021 (picha yakumbukumbu).
Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sissi wakati wa ziara yake nchini Sudan Machi 6, 2021 (picha yakumbukumbu). © AP

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi sasa anaonya kuwa njia zote zipo wazi baada ya mazungumzo ya hivi punde kuhusu hatua ya Ethiopia kujenga bwawa kubwa la umeme na kutumia maji ya mto Nile, kutozaa matunda

Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo hayo yalimalizilka siku ya Jumanne jijini Kinshasa bila ya pande zote tatu, ikiwemo Sudan kushindwa kupata makubaliano yoyote.

Misri na Sudan zimeishtumu, Ethiopia kwa kutokuwa na utashi wa kisiasa kutatua mzozo huo.

Ethiopia inasisitiza kuwa haitishwi na itaendelea na mpango wake wa kujaza bawa hilo kwa kutumlia maji ya mto Nile, hukju Waziri wake wa Maji Seleshi Bekele akisema hakuna haja ya kuingia kwenye vita.

"Hakuna haja ya kuingia kwenye vita ambavyo havistahili. Vita haviwezi kuanza kwa sababu ya maji. Maji yataendelea kuja. Hatujui ksho itakuwaje, kwa hivyo mawazo kama hayo yanastahiki kukoma kwa sababu, fikra kama hizo hazisaidia nchi yoyote," amesema Waziri wa maji wa Ethiopia, Seleshi Bekele.