MISRI

Rais wa Rwanda akaribisha ripoti ya Ufaransa kuhusu mauaji ya kimbari ya 1994

Rais Paul Kagame akihutubia wajumbe wakati wamaadhimisho ya kumbukumbu ya mauaji ya halaiki ya mwaka 1994  katikajengo la Kigali Arena, Kigali, huko Kigali, Rwanda Aprili 7, 2021.
Rais Paul Kagame akihutubia wajumbe wakati wamaadhimisho ya kumbukumbu ya mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 katikajengo la Kigali Arena, Kigali, huko Kigali, Rwanda Aprili 7, 2021. REUTERS - JEAN BIZIMANA

Rais wa Rwanda Paul Kagame, amesema ripoti ya wanahistoria wa Ufaransa kuwa nchi hiyo inawajibika na mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini humo mwaka 1994 na kusababisha vifo vya watu 800,000 wengi wao wakiwa Watustsi ni haut muhimu.

Matangazo ya kibiashara

“Tunakaribisha ripoti hii kwa sababu inaashiria hatua muhimu kuhusu uelewa wa pamoja kuhusu kilichotokea, inaashiria mlabadiliko na matamanio.  Jaribio la kipi,ndi kirefu la baadhi ya maafisa wa Ufaransa kukataa kuajibika kumesababisha madhara makubwa. Historia ilipotoshwa ili kuhusu ripoti ya doublé genocide na ile ya mapping.”

Ripoti hiyo ilikabidhiwa kwa rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, na kuishtumu nchi hiyo kwa kutofanya vya kutosha kuzuia mauaji hayo.

Akizungumza mbele ya viongozi mashuhuri mjini Kigali, siku ya kwanza ya wiki ya kumbukumbu ya mauaji hayo, Kagame amesema ni jambo zuri kusonga mbele kwa kufahamu kile kilichotokea, ikiwa ni miaka 27 tangu mauaji hayo yaliyoushutua ulimwengu.

Kagame amesisitiza tafsiri ya serikali yake ya matokeo ya uchunguzi wa tume ya Ufaransa kwamba rais wa Ufaransa wakati huo Francois Mitterand alifahamu mauaji ya halaiki ya Watutsi yalikuwa yakipangwa na washirika wake nchini Rwanda, lakini akaendelea kuwaunga mkono kwa sababu aliamini yalikuwa muhimu kwa nafasi ya Ufaransa katika siasa za kikanda. Hii ni mara ya kwanza Kagame kuizungumzia ripoti ya mauaji ya halaiki ya Ufaransa iliyotolewa mwezi Machi.

Rwanda imeingia katika kumbukumbuku ya miaka 27 tangu kutokea kwa mauaji hayo mabaya.