SUDAN

Sudan: idadi ya waliouawa Darfur Magharibi yaongezeka hadi 132

Makabiliano yaliyozuka kati ya kabila la kiarabu na kundi la jamii ya wasio waarabu la Massalit kwenye eneo la El Geneina yamesabibaisha vifo vya zaidi ya watu 100 na kujeruhi wengine zaidi ya 130.
Makabiliano yaliyozuka kati ya kabila la kiarabu na kundi la jamii ya wasio waarabu la Massalit kwenye eneo la El Geneina yamesabibaisha vifo vya zaidi ya watu 100 na kujeruhi wengine zaidi ya 130. © AFP

Hali sasa ni "tulivu" huko El-Geneina, mji mkuu wa Darfur Magharibi, unaokabiliwa na mapigano ya kikabila tangu Jumamosi. Mkuu wa mkoa huu unaopakana an Chad Mohamed abdalla Douma, ametangaza leo Alhamisi Aprili 8 kwamba idadi ya waliouawa sasa imefikia 132. Hakuna "mapigano tena" lakini "uporaji" unaendelea, ameongeza

Matangazo ya kibiashara

"Wanamgambo" walioushambulia mji huo walikuja wakitokea "nchi jirani kama vile Chad na Libya" na walitumia "silaha za kivita", amebaini Mohamed Abdallah Douma.

Mapigano hayo yalizuka wakati "kundi lenye silaha lilishambulia raia walipokuwa wakienda mjini", na kuua watatu, afisa huyo amesema. Umoja wa Mataifa, kwa upande wake, ulilikuwa umebaini "mapigano kati ya kabila la Al-Massalit na makabila ya Kiarabu".