DRC

Watu wa asili kupewa haki zote wanazopewa jamii zingine DRC

Makao makuu ya Bunge, Kinshasa, DRC.
Makao makuu ya Bunge, Kinshasa, DRC. RFI/Sonia Rolley

Bunge la Kitaifa nchini DR Congo limepiga kura Jumatano juu ya muswada ambao unaondoa ubaguzi dhidi ya watu wa asili waliotengwa zamani. Kuanzia huduma ya bure za afya hadi ada ya mahakama na hata gharama za elimu ya sekondari watapewa kama watu kutoka jamii zingine nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Licha ya Muswada huo kupitishwa bungeni bado haujapitia katika baraza la Seneti kwa hatua ya pili kabla ya kutangazwa na Rais Felix Tshisekedi, lakini hata hivyo waanzilishi wake wana matumaini kwa hatua zitazofuata.

Haya ndio matumaini yaliyochochewa na mbunge Rubin Rachidi, mlinzi wa mradi. Pia ni kilele cha kazi iliyochukua zaidi ya miaka 10, mapambano ya muda mrefu kwa shirika lisilo la kiserikali la Dynamique des groupes des peuples autochtones (DGPA)(DGPA.

Kati ya wabunge 383 waliokuwepo katika kikao hicho, ni mmoja pekee ndie aliyepinga bila hata hivyo kutoa sababu zake.

Kwa sheria hii, inatarajiwa kwamba mfuko wa kitaifa wa maendeleo kwa jamii ya mbilikimo utaundwa kwa ajili ya  utekelezaji wa sheria hiyo. Nchini DRC, sheria nyingi hupitishwa bila hata hivyo kutekelezwa kwa sababu ya ukosefu wa kifedha