BENIN

Benin: Hali ya wasiwasi yatanda siku mbili kabla ya uchaguzi

Huko Savè, Benin, waathiriwa wa maandamano hayo walipelekwa katika kituo cha afya Aprili 8, 2021. Watu wawili walifariki baada ya kupigwa risasi na vikosi vya usalama.
Huko Savè, Benin, waathiriwa wa maandamano hayo walipelekwa katika kituo cha afya Aprili 8, 2021. Watu wawili walifariki baada ya kupigwa risasi na vikosi vya usalama. AFP - YANICK FOLLY

Tangu mwanzoni mwa juma, maandamano yameongezeka nchini kote Benin ili kumpinga rais anayemaliza muda wake, Patrice Talon, ambaye ni mgombea wa uchaguzi dhidi ya wagombea wengine wawili wanaochukuliwa kuwa hawana ushawishi wowote.

Matangazo ya kibiashara

Huko Savè, wilaya iliyo katikati mwa nchi, Alhamisi ilikuwa katika hali ya wasiwasi: wanajeshi waliingilia kati kuondoa vizuizi kwenye barabara kuu ya Parakou, wakifyatua risasi za moto kwa waandamanaji na kuua wawili.

Idadi ya vifo imeongezeka. Vyanzo vya ndani vinaripoti kifo cha pili huko Savè. Mtu huyo aliyefariki dunia ni mmoja wa waliojeruhiwa, siku ya Alhamisi. Kufikia sasa ripoti zinasema kuwa watu wawili walifariki dunia na wanne waliruhiwa katika eneo hilo. Vyanzo rasmi pia vinaripoti majeraha kwa upande wa jeshi.

Jiji hilo, lililoko kilomita 250 kaskazini mwa Cotonou, sasa linaonekana kama mji unaokabiliwa na machafuko. Watu wamelazimika kusalia manyumbani, hakuna masoko, hakuna burudani. Kuna hali ya watu kutotoka nje. Jeshi bado lipo, linaendelea kukagua barabara ili kuzuia vizuizi zaidi.