CHAD

Chad: Viongozi kadhaa wa vyama vya siasa na wafuasi wao wakamatwa

(Picha ya kumbukumbu) Mahakama katika mji wa Ndjamena, Chad.
(Picha ya kumbukumbu) Mahakama katika mji wa Ndjamena, Chad. AFP/Pascal Guyot

Nchini Chad, Wizara ya Mambo ya Ndani imetangaza kukamatwa kwa viongozi kadhaa wa vyama vya siasa na wafuasi wao ambao wanashtumiwa kutaka kuvuruga uchaguzi wa urais wa siku ya Jumapili.

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa iliyotolewa Alhamisi jioni kufuatia tahadhari za upinzani zinazoonyesha kukamatwa kwa viongozi kadhaa wa maandamano, Wizara ya Usalama wa Umma imetangaza kuvunjwa kwa mtandao wa kigaidi.

Watu watano, viongozi wanne wa vyama vidogo vya kisiasa na kiongozi mmoja wa chama cha kiraia wamekamatwa. Wote ni kutoka muungano ambao ulitoa wito wa kususiwa kwa uchaguzi wa Jumapili siku moja iliyopita na kutoa wito wa kufanyika kwa maandamano leo na kesho Jumamosi.

Kulingana na afisa wa muungano huo, viongozi hawa walikuwa wamekusanyika kujadili juu ya mpango wa kususia, wakati karibu saa kumi  alaasiri, magari kumi  ya polisi yaliwasili eneo walikokuwa wakifanyia mkutano wao na kuwakamata.