DJIBOUTI

Wadjibouti wamchagua rais wao mpya

Mwanamke anaingia kwenye kituo cha kupigia kura huko Djibouti, Aprili 2016.
Mwanamke anaingia kwenye kituo cha kupigia kura huko Djibouti, Aprili 2016. AFP - KARIM LEBHOUR

Wananchi wa Djibouti wamepiga kura Ijumaa hii kumchagua rais wao, kura ambayo Ismaël Omar Guelleh anayemaliza muda wake, katika nchi hii ndogo ya kimkakati katika Pembe la Afrika, anagombea kwa awamu ya tano na, kinadharia, ya mwisho.

Matangazo ya kibiashara

Baadhi ya wapiga kura 215,000 waliojiandikisha (kati ya idadi ya watu 990,000) wameweza kwenda kwenye vituo vya kupigia kura kuanzia saa 6 asubuhi hadi saa 7 kuamua kati ya wagombea wawili katika uchaguzi huo.

Ismael Guelleh, mwenye umri wa miaka 73, amekuwa madarakani kwa miaka 22 katika nchi hii ndogo ambayo anatawala kwa mkono wa chuma na ambaye msimamo wake wa kimkakati ameweza kutumia, kwenye mipaka ya Afrika na Uarabuni.

Visa vya mambukizi ya virusi vya Corona vyavunja rekodi

Wakati wa kampeni ya uchaguzi, mikutano yake ilikusanya maelfu ya wafuasi wake waliovalia barakoa na ambao hawakuwa na barakoa, licha ya wimbi la maambukizi ya Covid-19, na hivi sasa visa karibu 200 vyaripotiwa kila siku na asilimia 23% ya vipimo kila siku.

Mbele yake, mgombea mwingine pekee ni Zakaria Ismail Farah, mwenye umri wa miaka 56, mfanyabiashara ambaye ameingia kwenye siasa hivi karibuni na ambaye amefanya mikutano michache ya kampeni ambayo haikiuwa na hamasa.

Kwa kukosekana kwa viongozi wa kihistoria wa upinzani, ambao walisusia kura, nafasi ya mshindani huyo asiejulikani kwa umma ni ndogo dhidi ya "IOG", Ismael Omar Ghelle ambaye alishinda na zaidi ya 75% ya kura kila uchaguzi wa rais alioshiriki.