DRC

Watu zaidi ya 8,000 wauawa Beni na katika mkoa wa Ituri

Rais wa Cenco, Askofu Mkuu Marcel Utembi (kushoto) na msemaji wa baraza hilo la Maaskofu Padre Donatien Nshole (kulia)
Rais wa Cenco, Askofu Mkuu Marcel Utembi (kushoto) na msemaji wa baraza hilo la Maaskofu Padre Donatien Nshole (kulia) AFP - JUNIOR D.KANNAH

Maaskofu nchini DRCongo wameonya kuwa Zaidi ya watu 6,000 wameuawa katika mkoa wa Beni tangu 2013 na zaidi ya 2,000 katika jimbo jirani la Ituri mnamo 2020, katika ghasia zilizotokea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Matangazo ya kibiashara

Padri Donatien Nshole, msemaji wa maaskofu, katika mkutano na waandishi wa habari huko Kinshasa amesema Vurugu zinazoendelea zimesababisha mauaji ya zaidi ya watu 6,000 huko Beni tangu 2013 na zaidi ya 2,000 huko Bunia mwaka 2020 pekee.

Kulingana na ripoti hiyo, Katika maeneo ya Beni, mkoa wa Kivu Kaskazini, na katika mkoa jirani ya Ituri, "pia kuna watu wasiopungua  milioni 3 waliokimbia makazi yao na karibu watu 7,500 wametekwa nyara.

Padre Nshole aliwasilisha ujumbe ambao wakuu wa kanisa katoliki ncini Kongo walishutumu "kukaliwa kwa ardhi, unyonyaji haramu wa maliasili, utajiri usiofaa, Kuyafanya maeneo hayo yawe ya kiislam na kupuuza uhuru wa kidini".

Kulingana na chanzo hiki, raia waliotoroka baada ya kutekwa nyara na wanachama wa Kikundi cha Waislamu wa Uganda cha Jeshi (ADF) walidai "kulazimishwa kufuata Uislamu".

Nyumba kadhaa zachomwa moto

Maaskofu hao pia walilaani uchomaji wa nyumba na vijiji, uharibifu na kufungwa kwa shule na vituo vya afya, upekuzi wa majengo ya utawala, uporaji wa wanyama, mashamba na mazao katika mkoa huu wa mashariki mwa nchi.

Mnamo Januari, ujumbe wa maaskofu kutoka Chama cha Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika ya Kati (Aceac) na Mkutano wa Kitaifa wa Maaskofu wa Kongo (Cenco) ulifanya ujumbe wa kichungaji katika majimbo ya Goma, Butembo-Beni (Kaskazini- Kivu) na Bunia (Ituri).