ALGERIA

Algiers yataka Paris kukarabati maeneo ya majaribio ya nyuklia ya Ufaransa

"Hatari": Bango hili lililoandikwa "hatari" kwa Kiarabu ambalo liliwekwa katika jangwa la Algeria - katika mkoa wa Tamanrasset - linaashiria hatari ya eneo hili kufuatia majaribio ya nyuklia ya Ufaransa mapema katika miaka ya 60.
"Hatari": Bango hili lililoandikwa "hatari" kwa Kiarabu ambalo liliwekwa katika jangwa la Algeria - katika mkoa wa Tamanrasset - linaashiria hatari ya eneo hili kufuatia majaribio ya nyuklia ya Ufaransa mapema katika miaka ya 60. AFP/Fayez Nureldine

Algeria imeomba msaada kutoka Ufaransa kukarabati maeneo ya majaribio ya nyuklia ya Ufaransa ambayo yalifanyika Algeria miaka 60 iliyopita. Ombi hilo lilitolewa wakati wa mkutano ambao haukutangazwa ambao ulifanyika Algiers kati ya mkuu wa jeshi la Algeria Said Chanegriha na mwenzake wa Ufaransa Jenerali François Lecointre siku ya Alhamisi.

Matangazo ya kibiashara

Faili ya jaribio la nyuklia ni moja wapo ya mizozo mikuu ya kumbukumbu kati ya Algiers na Paris. Ufaransa, mamlaka ya zamani ya kikoloni nchini Algeria, ilifanya majaribio 17 ya nyuklia katika Sahara ya Algeria kati ya mwka wa 1960 na 1966.

Algiers imebaini kwamba Ufaransa lazima "ikiri makosa yake ya kihistoria na itowe fidia kwa Sahara ya Algeria". "Matukio haya hayajafutwa kutoka kwa kumbukumbu" alionya rais wa Algeria mwezi uliopita.

Wakati wa mkutano kati ya wakuu wawili wa majeshi ya Algeria na Ufaransa, Jenerali Chanegriha alizungumzia suala hili. "Nataka tatizo kuhusiana na maeneo ya zamani ya majaribio ya nyuklia na majaribio mengine katika Sahara ya Algeria yajadiliwe katika kamatiya mseto kati ya Algeria na Ufaransa wakati wa kikao cha 17, kilichopangwa kufanyika Mei (2021), ambapo tunasubiri msaada kutoka Ufaransa, kwa kusaidia moja kwa moja usimamizi wa shughuli za ukarabati wa maeneo ya Reggane na Ain Akker. Pia, kuwa na ramani za hali ya juu ili kufafanua maeneo yaliyoathiriwa na uchafu wa nyuklia au kemikali. "

Wakuu hao wawili wa majeshi pia walijadili "hali ya ushirikiano wa kijeshi kati ya nchi hizo mbili" na kubadilishana maoni juu ya maswala yenye maslahi ya pamoja: mgogoro wa Sahel na vita dhidi ya kitisho cha jihadi ni miongoni mwa maswali hayo.