DRC

Utafiti: Mtu mmoja kati ya watatu aliyeathiriwa na uhaba mkubwa wa chakula DRC

Watoto walioyatoroka makaazi yao kutoka Ituri katika kambi huko Bunia, Aprili 9, 2018.
Watoto walioyatoroka makaazi yao kutoka Ituri katika kambi huko Bunia, Aprili 9, 2018. REUTERS/Goran Tomasevic

Ukosefu wa usalama, watu kuyatoroka makazi yao, makataa yakudhibiti virusi vya Corona ... Kwa sababu hizi zote, hali ya chakula inazidi kuzorota nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na hii inatia wasiwasi Umoja wa Mataifa. Zaidi ya watu milioni 27 wako hatarini kukabiliwa na njaa.

Matangazo ya kibiashara

Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa, WFP, na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) wamefanya utafiti kati ya wakaazi milioni 60 wa DRC, ikiwa ni pamoja na maeneo ya mijini.

Kulingana na utafiti huu, zaidi ya watu milioni 27, au karibu mmoja kati ya watu watatu nchini DRC, wako katika hatua ya 3 na 4 ya uhaba mkubwa wa chakula, ni kusema hatua zinazotangulia njaa, amesema Nourou Macki Tall, Naibu Mwakilishi wa FAO nchini DRC. Hii ni mara tatu zaidi ya miaka mitatu iliyopita.

"Sehemu ya njia wanayotumia mikakati ya kuishi ni kula angalau mlo mmoja kwa siku, na ndani ya familia kuna vipaumbele, ni kusema ninani anayepaswa kula. Ni wakimbizi wa ndani na wakimbizi ambao walioathirika zaidi, pamoja na watu wengine ambao tayari wako katika hali mbaya, kutokana hasa na athari inayosababishwa na Covid-19. Watu hawawezi kutofautisha vyanzo vyao vya mapato ili kuweza kupata masoko ikiwa katika masoko hayo hayo kuna ukosefu wa usalama, hasa katika mikoa iliyoathirika zaidi, Kivu Kaskazini na Kivu Kusini ”, Naibu Mwakilishi wa FAO nchini DRC amebaini.

Msaada wa haraka wa chakula na kuokoa kampeni ya kilimo

"Hatua ya kwanza ya haraka ni msaada wa haraka wa chakula kwa njia ya chakula au pesa taslimu, ambapo kuna masoko yanayofanya kazi. Hatua ya pili ya haraka ni kuwapa watu hawa njia za kuokoa msimu wa kilimo mnamo mwezi Mei na msimu wa kilimo mnamo mwezi Septemba. Zaidi ya 80% ya wazalishaji hawana mbegu bora, ”ameongeza Nourou Macki Tall.