BENIN

Benin: Wakaazi wa Cotonou wanatarajia uchaguzi wa "amani"

Wapiga kura wanatarajia kura "ya amani" katika uchaguzi huu wa urais (Picha ya kumbukumbu).
Wapiga kura wanatarajia kura "ya amani" katika uchaguzi huu wa urais (Picha ya kumbukumbu). © YANICK FOLLY/AFP

Wananchi wa Benin wanapiga kura leo Jumapili Aprili 11 baada ya kampeni iliyogubikwa na machafuko mabaya katikati na kaskazini mwa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Mji mkuu wa kiuchumi ulinusurika na ghasia mbaya ambazo zilitokea mwishoni mwa kampeni za uchaguzi katikati na kaskazini mwa Benin.

Mabango ya kampeni yaliyo na picha ya Patrice Talon na wapinzani wake wawili yametoweka kwenye mitaa ya Cotonou, kama sheria inavyotaka baada ya kampeni ya uchaguzi. 

Hali hii iliyokuwa ikiendelea nchini Benin imefanya watu wengi kuwa na hofu ya nchi hiyo kukumnbwa na machafuko mabaya zaidi.

Rais anayemaliza muda wake Patrice Talon ambaye anawania kwa muhula wa pili, anapambana katika uchaguzi huo na wainzani kadhaa lakini wawili, Alassane Soumanou na Corentin Kohouéndio, wanaonekana kuwa na shinikizo kubwa dhidi yake.