MISRI

Katika mvutano kamili na Ethiopia, Misri yajiunga na Uganda

Boti za uvuvi kwenye Mto Nile huko Entebbe, Uganda, 2008.
Boti za uvuvi kwenye Mto Nile huko Entebbe, Uganda, 2008. AFP

Uganda na Misri wiki hii ziliitia saini makubaliano ya kugawana taarifa za kijasusi za kijeshi "kupambana na ugaidi." Makubaliano haya kati ya nchi hizi mbili zinachangia Mto Nile yanakuja katikati ya mzozo kuhusiana na matumizi ya maji ya mto huo, kutokana na bwawa la Renaissance lililojengwa na Ethiopia.

Matangazo ya kibiashara

"Kinachoathiri Waganda kitaathiri Misri," Naibu Mkuu wa idara ya ujasusi wa kijeshi kutoka Misri Sameh Saber El-Degwi amesema katika taarifa ya jeshi la Uganda makubaliano yaliyosainiwa Jumatano. Nchi hizi mbili huchangia maji ya Mto Nile.

Makubaliano ya kijeshi ambayo hayahusiani na kufeli kwa majadiliano kuhusu bwawa kubwa la Renaissance, amebainisha Deo Akiiki, msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Uganda: "Kutiwa saini kwa makubaliano haya kunafuatia mkutano uliofanyika mwezi Desemba na idara ya upelelezi ya Misri. Ijapokuwa mivutano iko kati ya Misri, Ethiopia na Sudan, hii hawezi kutuzuia kushirikiana na Misri. Taarifa za kijasusi ambazo tutapeana na Cairo zitafaidi bara lote na washirika wetu wa Ethiopia hawatakiwi kuwa na wasiwasi. "

Ushirikiano wa kushangaza

Hata hivyo ni ushirikiano wa kushangaza kwa baadhi ya wachambuzi, ambao wanasema Uganda kwa muda mrefu imekuwa mshirika wa Ethiopia, adui wa Misri.

Mtazamo huu unakosolewa na Fadi Comair, mtaalamu wa elimu ya maji katika shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO: "Ethiopia inajizuia, kwa sababu kuna uchaguzi unatarajiwa kufanyika nchini humo na serikali inajaribu kuhamasisha raia wake kuhusiana na jambo muhimu ambalo ni bwawa hilokubwa la Rennaissance. Mazungumzo ya moja kwa moja yatalazimika kuanza tena, kwa sababu ikiwa ujazaji huu utafanyika bila ushirikiano kati ya mataifa, kwa bahati mbaya kuna hatari ya kuwa na mzozo karibu na Mto Blue Nile. "

Duru mpya ya mazungumzo ya pande tatu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilishindwa kufikia makubaliano Jumanne (Aprili 6).