CAR

CAR: Jeshi na washirika weke wadhibiti mji wa kimkakati wa Kaga-Bandoro

Askari wa jeshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati (FACA), Agosti 4, 2018, huko Berengo. (Picha ya kumbukumbu)
Askari wa jeshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati (FACA), Agosti 4, 2018, huko Berengo. (Picha ya kumbukumbu) FLORENT VERGNES / AFP

Mamalaka nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati, wanakaribisha operesheni ya jeshi na washirika wake, hasa Urusi, kwa kuweza kudhibiti mji wa Kaga-Bandoro.

Matangazo ya kibiashara

Mji huu wa kimkakati wa kibiashara, kilomita 300 kaskazini mwa mji wa Bangui, umekuwa mikononi mwa makundi yenye silaha tangu mwaka 2014.

Ilikuwa muda mfupi kabla ya saa 11 jioni Jumamosi Aprili 10 ambapo vikosi vya jeshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati na washirika wake waliingia katika mji wa Kaga-Bandoro. Waliingia katika mji huo  kwa makundi mawili, kulingana na vyanzo vya usalama. Kundi la kwanza lilipitia eneo la Mbrès, mashariki, kundi la pili lilitokea katika eneo la Dekoa, kusini mwa mji huo saa chache baadaye.

"Walipofika, milio mikali ya risasi ilisikika, lakini ni kama tu hakukuwa na mapigano," kimesema chanzo katika eneo hilo. Operesheni hiyo ya kijeshi ilitangazwa na mamalaka kama lengo muhimu.

Siku ya Jumapili, jeshi na washirika wake kwa pamoja walifanya shughuli za upekuzi katika maeneo kadhaa ya jiji. "Wanatafuta silaha na wamekamata watu kadhaa," kimesema chanzo kutoka mashirika ya kiraia.

Mbinu ya waasi ya kurudi nyuma

Sehemu ya waasi ambao walikuwa wakishikilia mji wa Kaga-Bandoro tangu mwaka 2014 waliondoka mji huo hivi karibuni, kulingana na vyanzo vya usalama. Kwa wale ambao walikuwa bado wapo, waliondoka Jumamosi jioni bila kupigana, kuelekea kaskazini, katika mji ya Kabo na Batangafo, kulingana na vyanzo kadhaa. Wengi wao ni wapiganaji wa kundi la UPC la al-Khatim, kutoka kundi la zamani la Seleka.