DRC

FARC yadai kuuwa waasi watano Kivu Kusini

Jeshi ladrc, FARDC, wanaendelea kukabiliana na makundi yenye silaha mashariki mwa nchi hiyo.
Jeshi ladrc, FARDC, wanaendelea kukabiliana na makundi yenye silaha mashariki mwa nchi hiyo. REUTERS/Goran Tomasevic

Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, limesema limewauwa waasi watano mwishoni mwa wiki iliyopita karibu na maeneo ya Minembwe Mashariki mwa nchi hiyo, huku watu wengine 12 wakiuawa katika eneo la Daraja la Semuliki, katika jimbo la Kivu Kaskazini.

Matangazo ya kibiashara

Utovu wa usalama Mashariki mwa nchi hiyo umesababisha wananchi kuandamana kuonesha hasira zao dhidi ya jeshi la serikali na lile la Umoja wa Mataifa MONUSCO.

Watu ameyatoroka makaazi yao kutokana na mdroro wa usalama wakihofia kuuawa na makundi ya watu wenye silaha, wakaazi karibu ote wamehama katika eneo la Ruwenzori wilayani.

Vyanzo kutoka eneo hilo vinabaini kwamba watu wanarudi mchana kujishughulisha na shughuli mbalimbali na usiku wanakwenda maeneo salama.