BENIN

Zoezi la kuhesabu kura laanza Benin

Kura zikihesabiwa katika kituo cha kupigia kura katika mkoa wa Cadjehoun huko Cotonou, Jumapili hii, Aprili 11, 2021..
Kura zikihesabiwa katika kituo cha kupigia kura katika mkoa wa Cadjehoun huko Cotonou, Jumapili hii, Aprili 11, 2021.. © Aurore Lartigue/RFI

Nchini Benin, baada ya wananchi kupiga kura siku ya Jumapili kumchagua rais, katika uchaguzi uliosusiwa na vyama vya upinzani kupinga hatua ya rais Patrice Talon kuwania tena kuongoza taifa hilo kwa miaka mitano, kura zimeanza kuhesabiwa.

Matangazo ya kibiashara

Idadi ya wapiga kura ilikuwa ndogo ikilinganishwa na uchaguzi uliopita, kwa mujibu wa ripoti ya mashirka ya kiraia, na rais Talon mfanyibiashara tajiri anatarajiwa kushinda uchaguzi ambao wapinzani tayari wanadai kuwa hauwezi kuwa huru na haki.

Baada ya kupiga kura, rais Talon alitoa wito kwa wananchi wa taifa hilo kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi hilo.

“Ikiwa nina ujumbe wowote kwa wananchi wenzangu, ni kuwa nijukumu la kila mmoja kwenda kushiriki kwenye zoezi hili licha ya taarifa za kupotosha wanazozipata tukabiliane na mvua na jua kwenda kutekeleza jukumu hili muhimu.”