BURKINA FASO

Kifo cha Thomas Sankara: Mahakama yaamua kumshtaki rais wa zamani Compaoré

Kaburi la Thomas Sankara huko Ouagadougou, Burkina Faso.
Kaburi la Thomas Sankara huko Ouagadougou, Burkina Faso. Siegfried Forster / RFI

Mahakama ya kijeshi nchini Burkina Faso imetoa uamuzi juu ya kushtakiwa kwa rais wa zamani Blaise Compaoré kwa kuhatarisha usalama wa nchi, kushiriki katika mauaji na kuficha maiti katika kesi ya mauaji ya hayati rais Thomas Sankara.

Matangazo ya kibiashara

Gilbert Diendéré, mshirika wa karibu wa zamani wa Blaise Compaoré, pia anmeshtakiwa. Jumla ya watu 14 wanatakiwa kufika mahakami kuhusiana na kesi hii.

 

Rais wa zamani Blaise Compaoré atalazimika kufika mahakamani kujieleza kuhusu shutma zinazomkabili katika kesi hiyo. Kulingana na uamuzi wa mahakama, kuna mashtaka ya kutosha dhidi ya kiongozi huyo wa zamani kwa kuficha maiti na mahakama ina waranti wa kukamatwa wa kimataifa dhidi yake.

Mkuu wa kikosi kilichotekeleza mauaji akabiliwa na mashitaka makubwa

Mhakama pia ina waranti wa kukamatwa wa Hyacinthe Kafando, anayeshtakiwa mauaji na kuhatarisha usalama wa nchii. Anayedaiwa kuwa mkuu wa kikosi kilichotekeleza mauaji ya Kapteni Thomas Sankara na wenzake. Ameshtakiwa pia katika kesi hii, Jenerali Gilbert Diendéré, mshirik wa karibu wa zamani wa Blaise Compaoré. Katika kesi hiyo, watu kumi na wanne wanatakiwa kuripoti mahakamani.

Wakati huo huo, mahakama ya kijeshi imeagiza kuwekwa kizuizini kwa wale wote ambao mashtaka yao yamethibitishwa, ingawa hakuna tarehe ya kesi iliyotangazwa. Hata hivyo waranti za kukamatwa zimehifadhiwa dhidi ya wale walio nje ya nchi.