Mfungo wa Ramadhan waanza chini ya masharti ya kupambana na Corona

Msikiti wa Kibuli katika mji mkuu wa Uganda Kampala, mwaka 2020.
Msikiti wa Kibuli katika mji mkuu wa Uganda Kampala, mwaka 2020. © Wikimedia Commons CC-BY-SA 4.0 Alvinategyeka

Waumini wa dini ya Kislamu wanaanza mfungo wa Ramadhan leo Jumanne,huku mataifa mengi yakiwa yamejeresha masharti ya kupambana na maambukizi ya Corona.

Matangazo ya kibiashara

Mfungo wa Ramadhan wa mwezi moja ni mojawapo ya nguzo ya dini ya Kislamu,umeanza  chini ya masharti  ya kupambana na Corona kwa mwaka wa pili.

Barani Afrika nchi kama Misri, Tunisia, Kenya, Uganda zimezuia ibada kwenye misikiti ili kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo. 

Katika mataifa ya mashariki ya kati, mbali na kukumbwa na  kasi ya maambukizi ya Corona , yanapambana na changamoto ya ukosefu wa nafasi za ajira, mfumuko wa bei za bidhaa muhimu na familia nyingi huenda zikashindwa kujipatia chakula wakati huu wa Ramadhan.

Mkurugenzi wa shirika la afya duniani, ukanda wa Meditereanean Ahmed AL Mandhari amesema mwaka uliopita, baada ya Ramadhan, nchi nyingi zilishuhudia ongezeko la maambukizi na vifo vingi na hivyo ni muhimu kwa masharti ya kudhibiti maambukizi ya Corona kuzingatiwa mwaka huu.