BENIN

Benin: CENA yamtangaza Patrice Talon mshindi wa uchaguzi wa urais

Kulingana na matokeo ya awali yaliyotangazwa na CENA, Rais Patrice Talon amechaguliwa tena kwa kura milioni 2.
Kulingana na matokeo ya awali yaliyotangazwa na CENA, Rais Patrice Talon amechaguliwa tena kwa kura milioni 2. AFP - PIUS UTOMI EKPEI

Kulingana na matokeo ya muda yaliyotangazwa Jumanne jioni na Tume huru ya Uchaguzi (CENA), Rais wa Benin Patrice Talon amechaguliwa tena katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais kwa asilimia 86.57 ya kura na kiwango cha ushiriki kilifikia 50.17%.

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na takwimu za awali zilizotangazwa na CENA, Patrice Talon na mgombea mwenza Mariam Chabi Talata wameshinda uchaguzi wa urais kwa asilimia 86.57% ya kura zilizopigwa, sawa na kura milioni 2 tu. Rais Talon "amepata kura nyingi zilizopigwa katika duru ya kwanza," imesema Tume ya Uchaguzi.

Soumanou na Hounkpè, kutoka chama cha FCBE, wameshika nafasi ya pili kwa 11.29% ya kura. Paul Hounkpè ameshutumu amelaani  udanganyifu mlkubwa uliogubika uchaguzi huo na kuvo kusababisha kushindwa kwao: “Haya ni matokeo ya awali. Kutokana na makosa kadhaa, tunakadiria kuwa tungelpata kura nyingi zaidi. Tunatumahi kuwa kura zetu zitarekebishwa upya. "

Matokeo haya ya awali yanatarajiwa kutumwa katika mahakama ya Katiba, yenye dhamana ya kutangaza matokeo ya mwisho ya kura.