UKRAINE

Ukraine: Joe Biden na NATO wapaza sauti dhidi ya Moscow

Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg ametoa wito kwa Moscow "kusitisha hatua zake za kijeshi dhidi ya Ukraine".
Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg ametoa wito kwa Moscow "kusitisha hatua zake za kijeshi dhidi ya Ukraine". AP - Francisco Seco

Wanachama wa Jumuiya ya kujihami ya nchi za Magharibi na rais wa Marekani wameionya Urusi katika jaribio la kumaliza mzozo mpya huko Ukraine na kujibu mazoezi ya kijeshi ya Urusi

Matangazo ya kibiashara

"Hatua ya kutumwa kwa idadi kubwa ya wanajeshi la Urusi kwenye mpaka na Ukraine haina sababu, haelezeki na inatia wasiwasi sana," ameshutumu Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg, baada ya mkutano na Waziri wa Mambo ya nje wa Ukraine Dmytro Kulebo, ambaye alikuja Brussels kutafuta msaada wa Jumuiya ya Mkataba wa Atlantiki dhidi ya kupelekwa kwa vikosi vya Urusi kwenye mpaka wa Ukraine.

"Urusi inapaswa kusitisha zoezi lae la kutuma vikosi vya jeshi kwenye mpaka na Ukraine, isitishe chokochoko zake na kusitisha hatua yake ya kijeshi ambayo inaweza kusababisha mgogoro mpya," ameongeza Jens Stoltenberg. Urusi lazima iheshimu ahadi zake za kimataifa. Msaada wa NATO kwa Ukraine haubadiliki. "

Urusi yashtmu NATO kwa hatua za "vitisho"

Wakati mzozo katika Donbass umeendelea kufukuta kwa wiki kadhaa, Kiev imeishutumu Moscow kwa kukusanya askari wake kwenye mipaka yake. Ilikadiria Jumatatu kuwa idadi ya wanajeshi hao imefikia 83,000, karibu nusu yao huko Crimea, peninsula iliyoambatanishwa na Urusi mnamo mwaka 2014. Urusi haikukanushamadai hayo yya kupelekwa kwa anajezhi wake katika eneo hilo, huku ikisisitiza kwamba "haijakutishia mtu yeyote" na ikishutumu "chkochoko" kutoka Ukraine.

Siku ya Jumanne, Waziri wa Ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu alithibitisha kupelekwa kwa wanajeshi katika maeneo ya magharibi na kusini mwa nchi hiyo, akisema ni jibu kwa vitendo vya "vitisho" vya NATO. Kulingana na Sergei Choïgou, wanajeshi waliotumwa kwa wiki tatu zilizopita - "makundi mawili ya jeshi na vitengo vitatu vya kikosi cha angani" - wanafanya "mazoezi ya kijeshi" ambayo yatadumu wiki mbili zaidi.