ETHIOPIA

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuujadili mzozo wa Tigray

Thousands have died in fighting Ethiopia's northern Tigray region
Thousands have died in fighting Ethiopia's northern Tigray region EDUARDO SOTERAS AFP/File

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, linatarajiwa kukutana leo kujadili mzozo wa jimbo la Tigray ,nchini Ethiopia, wakati serikali ya nchi ikieelea kukosolewa kuhusi jinsi inavyoshughulikia mzozo wa jimbo la Tigray.

Matangazo ya kibiashara

Kikao hicho kitaandaliwa kufuatia ombi la Marekani la kujadiliwa mzozo huo ambao umesababisha vifo vya mamia ya watu.

Mkuu wa mashirika ya kutoa msaada kwenye umoja huo Mark Lowcok anatarajiwa kuelezea mataifa 15, wanachama wa Baraza hilo kuhusu channgamoto za kuwafikia wakimbizi kuwapa misaada ya kibinadamu.

Kikao hiki kinakuja, baada ya Ethiopia kukiri kuwepo kwa vikosi vya Eritrea katika jimbo la Tigray na kuahidi kuwa vikosi hivyo vya nchi jirani vitaondoka.

Ripoti iliyotolewa na shirika la kimataifa la Amnesty Internatonal siku ya Jumatano, imelishtumu jeshi la Eritrea kwa kuwauwa watu watatu na kuwajeruhi wengine 19 baada ya kuwashambulia raia wa jimbo la Tigray.