MSUMBIJI

Wanamgambo wa kiislamu waenelea kuzusha hofu Msumbiji

Watu waliotoroka makaazi yao katika mji wa Palma na vyunga vyakena kukimbilia huko Pemba, Aprili 1, 2021.
Watu waliotoroka makaazi yao katika mji wa Palma na vyunga vyakena kukimbilia huko Pemba, Aprili 1, 2021. REUTERS - STRINGER

Watalaam wa maswala ya usalama wameonya kuwa wanajihadi walioshambulia mji wa Palma, kaskazini mwa Msumbiji, huenda wanapanga kutekeleza mashambulizi mengine.

Matangazo ya kibiashara

Onyo hili linakuja wakati huu kukiwa na kumbukumbu mbaya ya wanajjihadi hao wa Kiislamu kushambulia mji wa Palma tarehe 24 mwezi Machi na kusababisha maafa, huku maelfu ya wakaazi wa mji huo wakiyakimbia makwao.

Martin Ewi mtaalam wa masuala ya usalama kutoka kituo cha mafunzo ya usalama nchini Afrika Kusini, anaonya kuwa wanajihadi hao hawalali na wanapanga kutekeleza mashambulizi mengine.

Onyo hili linakuja wakati kukiwa na hofu pia kwenye vijiji vinavyopakana na nchi ya Tanzania kuwa huenda wanajihadi hao wakavuka mpaka.

Wiki iliyopita, wakuu wa nchi za Kusini mwa Afrika, SADC, walikutana mjini Maputo na kuapa kupambana na kundi hilo la kijihadi.