MSUMBIJI

Msumbiji: Mapigano mapya yazuka karibu na Palma

Hali ya usalama katika mji wa Palma bado ni wasiwasi.
Hali ya usalama katika mji wa Palma bado ni wasiwasi. © LUSA - João Relvas

Mapigano mapya yametokea katika mji wa Palma, katika jimbo la Cabo Delgado, kaskazini mashariki mwa Msumbiji. Mapigano hayo yametokea wiki tatu baada ya shambulio kubwa la wanajihadi ambalo lilisababisha vifo vya watu wengi na maelfu kuyatoroka makaazi yao.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi, hata hivyo, alidai wiki iliyopita kwamba wanajihadi "wafukuzwa" katika mji wa Palma na kwamba wengi miongoni mwao waliuawa.

Mji huo na mviunga vyake vinaonekana kuwa chini ya vitisho vya wanajihadi hao tangu mapigano mapya kuzuka huko Palma. Kulikuwa pia, kulingana na chanzo cha jeshi, mashambulio ya wakati mmoja dhidi ya maeneo mawili kwenye umbali wa kilomita 200.

TOTAL yaombwa kuendelea kufanya shughuli zake Palma

Operesheni mpya zilifanyaka zaidi ya wiki tatu baada ya makundi yenye silaha yaliyojiunga na kundi la Islamic State kuhatarisha usalama katika eneo hilo. Shambulio la Palma lilidumu kwa siku kadhaa na kuua watu kadhaa, kulingana na vyanzo rasmi.

Sehemu muhimu katika mkoa huo, Palma iko kilomita chache tu kutoka eneo kunakoendeshwa mradi mkubwa wa gesi unaosimamiwa na kampuni ya Ufaransa ya TOTAL. Tangu wakati huo kampuni hii ililazimika kufunga shughuli zake zote.

Kwa mara ya kwanza Alhamisi hii, Aprili 15, Waziri wa Ulinzi wa Msumbiji alizungumza akielezea kwamba "mradi huu unaoongozwa na TOTAL hautishiwi, na kwamba utaendelea".