TUNISiA

Wahamiaji wasiopungua 40 waangamia pwani ya Tunisia

Ukanda wa pwani karibu na mji wa bandari wa Sfax umekuwa mahali muhimu pa kuanzia safari yao kwa watu wanaokimbia mizozo na umaskini Afrika na Mashariki ya Kati na kutafuta maisha bora barani Ulaya.
Ukanda wa pwani karibu na mji wa bandari wa Sfax umekuwa mahali muhimu pa kuanzia safari yao kwa watu wanaokimbia mizozo na umaskini Afrika na Mashariki ya Kati na kutafuta maisha bora barani Ulaya. AP - Houssem Zouari

Wahamiaji wasiopungua 40 wamefariki dunia baada ya boti waliokuwemo kuzama katika pwani ya Tunisia wakati waliokuwa wakijaribu kuvuka Bahari ya Mediterania kuingia Italia, maafisa wa Umoja wa Mataifa na Tunisia wamesema

Matangazo ya kibiashara

Kikosi cha walinzi wa pwani ya Tunisia kufikia sasa wamepata miili 21, ambapo wote ni raia kutoka nchi mbalimbali za Afrika, na kuokoa watu watatu, maafisa wa Tunisia wamesema. Mtoto mmoja ni miongoni mwa watu waliofariki dunia.

"Boti lilizama wakati lilikuwa likivuka Bahari ya Mediterania, siku ya Alhamisi katika eneo la Sfax ... Kufikia sasa kikosi cha walinzi wa pwani ya Tunisia kimepata miili 21 na shughuli ya utafutaji inaendelea," mkurugenzi wa ulinzi wa raia wa Tunisia Mouard Mechri, ameliambia shirika la habari la REUTERS.

Ukanda wa pwani karibu na mji wa bandari wa Sfax umekuwa mahali muhimu pa kuanzia safari yao kwa watu wanaokimbia mizozo na umaskini Afrika na Mashariki ya Kati na kutafuta maisha bora barani Ulaya.

Mwezi uliopita, wahamiaji 39 walifariki kwenye pwani ya Sfax katika ajali kama hiyo.