DRC

DRC: Balozi za DRC zakabiliwa na matatizo ya kifedha

DRC kwa sasa ina balozi karibu sitini duniani.
DRC kwa sasa ina balozi karibu sitini duniani. AP - Riccardo De Luca

Balozi za DR Congo kote duniani zinakabiliwa na matatizo makubwa za kiutendaji. Baadhi ya balozi za nchi hiyo zinakabiliwa na malimbikizo ya hadi miezi 12 na kodi ambazo hazijalipwa na hatari ya kufukuzwa kwa baadhi ya zingine, au mishahara ambayo hilipwi tena.

Matangazo ya kibiashara

Hali hii imesababisha Waziri wa Mambo ya Nje, Marie Tumba Nzeza, kuonya katika vyombo vya habari akiomba kuhusika zaidi kwa serikali ya DR Congo ili kumaliza matatizo hayo.

Kwa mujibu wa mwandishi wetu Kinshasa, Patient Ligodi mchakato wa urekebishaji ulizinduliwa tangu Jumatatu, Aprili 12. Agizo hilo lilitolewa kwa Benki Kuu ya DRC. Kati ya kiasi kinachokadiriwa kuwa dola milioni 9, milioni 3 zitatolewa mwanzoni, kulingana na vyanzo kutoka Wizara ya Mambo ya nje.

Kipaumbele kitatengwa kwa kodi ili kuhifadhi picha ya nchi, kulingana na ofisi ya rais wa Jamhuri, ambapo Felix Tshisekedi alihusika kibinafsi.

Serikali kuchukua hatua ya kupunguza idadi ya balozi

Pamoja na matatizo haya ya kimazingira, serikali inatarajia kuchukua hatua sahihi. "Kuna haja ya wazi ya kuleta utulivu katika sekta hii," amesema afisa mwandamizi katika ofisi ya rais.

Nchi hiyo kwa sasa ina balozi karibu sitini duniani. Mageuzi yaliyotangazwa yanapaswa kujikita katika kupunguzwa kwa idadi hii kwa sababu za kibajeti. Kinshasa inataka kubadilisha sera yake ya kigeni kulingana na changamoto za sasa.