MALI

Mali: Mapigano mabaya yazuka kati ya Dozos na wanajihadi Djenné

Jeshi la Mali likipiga doria kwenye barabara inayounganisha mji wa Mopti na Djenné, katikati mwa Mali, Februari 28, 2020.
Jeshi la Mali likipiga doria kwenye barabara inayounganisha mji wa Mopti na Djenné, katikati mwa Mali, Februari 28, 2020. AFP - MICHELE CATTANI

Wakati wawindaji kutoka jamii ya Dozo na wanajihadi kutoka kundi la Katiba Macina wanaelewana katika mji wa Niono, wameendelea kukabiliana katika mji jirani wa Djenné katikati mwa Mali.

Matangazo ya kibiashara

Mapigano ya hivi karibuni yalisababisha vifo vya watu kadhaa, vijiji vimeteketezwa kwa moto na familia nyingi zimelazimika kuyatoroka makaazi yao.

Mzozo huo ulianza zaidi ya mwezi mmoja na nusu uliopita. Wanajihadi wa Katiba Macina, wakiongozwa na Amadou Kouffa na waliofungamana na JNIM (kundi lilanotetea Uislamu na Waislamu la Iyad Ag Ghaly, lenye mafungamano na AQMI), yanayopiga kambi katika eneo la Djenné kwa miaka kadhaa, yamekuwa yakiwaibia raia mifuko ya mchele kutoka vijiji vya maeneo hayo. Hii ni "zakat" (sadaka za Kiislamu) zilizotozwa kwa wakaazi. Siku hiyo, katikati ya mwezi wa Februari, wawindaji wa kijadi kutoka jamii ya Dozo walimua kuchukuwa sehemu ya mali hiyo.

Watu kadhaa wauawa

Baada ya makabiliano hayo visa vya ulipizaji kisasi viliripotiwa, mashambulio ya kuvizia yaliongezeka mwanzoni mwa mwezi huu na kufikia kilele katika siku nne zilizopita: vyanzo - maafisa wa usalama, serikali za mitaa, watu mashuhuri na viongozi wa jamii au mashirika ya kiraia - wamebaini kwamba mashambulizi hayo au mapigan hayo yalisababisa vifo vya watu weng, baadhi wanabaini vifo vya watu kumi, wengine thelathini, na wengine sitini wameuawa kwa upande wa wawindaji kutoka jamii ya Dozo, pamoja na waliojeruhiwa na wafungwa.