DRC

Mamlaka katika mkoa wa Kivu Kusini yashtumiwa kwa ufisadi

Bukavu, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kusini, mashariki mwa DRC.
Bukavu, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kusini, mashariki mwa DRC. Marine Gauthier / EyeEm

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, watu wasiopungua saba walijeruhiwa vikali kwenye uwanja wa michezo wa Funu mjini Bukavu Jana jumapili jioni wakati polisi ilisambaratisha mkutano ulioandaliwa na baadhi ya wabunge wa mkoa wa Kivu Kusini

Matangazo ya kibiashara

Katika mkutano huo walisema kwamba walitaka kuambia raia ukweli ila kabla mkutano kuanza, polisi ilisambaratisha watu waliotaka kushiriki mkutano.

« Kwa mshangao mkuu tulipokuwa pale tuliona maafisa wengi wa polisi. Ni watu 12 waliojeruhiwa vikali kabisa »

Wabunge hao wanashutumu gavana wa mkoa wa Kivu kusini Théo Ngwabidje kwa uongozi mbaya mkiwemo ufisadi na kushindwa kulinda usalama wa raia, wakisema kuwa tangu mwanzo wa mwaka huu wa 2021 visa zaidi ya 1300 vya ukosefu wa usalamavimeripotiwa katika mkoa wa Kivu Kusini.

Kwa upande wake gavana Ngwabidje wamelezea tukio hilo kutokana na sababu za kupambana dhidi ya maambukizi ya Covid-19 na pia kwamba mkutano huo haukujulishwa mapema kwa viongozi. Jordan Muke ni afisa wa chumba cha mawasiliano cha ofisi ya gavana wa mkoa wa kivu kusini :

« Mbunge ni mtu anayetakiwa kuheshimu sheria zote za nchi. Kwanza ingetakiwa kutoa taarifa kuhusu mkutano, na pia wakati huu wa nchini nyingi zinakabiliana na janga la Covid-19 inabidi watu waheshimu masharti yaliyowekwa»

Kusambaazwa kwa maandamano hayo kunakosolewa na mashirika mengi ya kiraia nchini DR Congo, yakionya kuwa janga la Corona lisiwe kisingizio kwa kuminya haki za raia.