MISRI

Misri: Kumi na mmoja waangamia katika ajali ya treni, karibu 100 wajeruhiwa

Watu hukusanyika katika eneo ambalo mabehewa yalipoteza mwelekeo na kusababisha ajali katika mkoa wa Qalioubia, kaskazini mwa Cairo, Misri Aprili 18, 2021.
Watu hukusanyika katika eneo ambalo mabehewa yalipoteza mwelekeo na kusababisha ajali katika mkoa wa Qalioubia, kaskazini mwa Cairo, Misri Aprili 18, 2021. REUTERS - MOHAMED ABD EL GHANY

Takriban watu kumi na mmoja wamefariki dunia na karibu 100 wamejeruhiwa katika ajali ya treni iliyotokea kaskazini mwa mji mkuu wa Misri Cairo hivi punde, wiki tatu baada ya treni mbili kugongana nchini  humo.

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na taarifa ya serikali, mabehewa manne ya treni kutoka Cairo kwenda Mansoura, kilomita 130 kaskazini mwa nchi, yalipoteza mwelekeo katika eneo la kilimo la Toukh. Sababu za ajali hazijajulikana.

"Watu kumi na moja wamefariki dunia na 98 wamejeruhiwa katika ajali ya treni huko Toukh", katika Delta ya Nile, kulingana na ripoti ya hivi punde kutoka kwa Wizara ya Afya. Majeruhi kumi na wanne wameweza kuruhusiwa kutoka hospitali.

Magari mengi ya wagonjwa yalitumwa katika eneo la ajali, kulingana na Wizara ya Afya. Wachunguzi walitumwa huko kujaribu kujua sababu.

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi amewaagiza wahandisi wa kijeshi kuchunguza mkasa huu mpya.

Kulingana na chanzo cha usalama, dereva wa treni na maafisa wengine wa treni wamekamatwa kwa kuweza kuhojiwa.