DRC

DRC: waziri wa zamani wa Elimu, Willy Bakonga, akamatwa Brazzaville

Willy Bakonga, waziri wa zamani wa Elimi DRC.
Willy Bakonga, waziri wa zamani wa Elimi DRC. eduquepsp.education

Waziri wa zamani wa Elimu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo anazuiliwa jijii Kinshasa baada ya kukamatwa Jumanne jioni katika mji mkuu wa Congo, Brazzaville, kwa ombi la Kinshasa.

Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Kinshasa inamshutumu kwa ubadhirifu, kulingana na shirika la habari la AFP likinukuu chanzo cha polisi.

"Willy Bakonga, Waziri wa zamani wa Elimu nchini DRC, alishuka Jumanne jioni kwenye ndege ya shirika la ndege la Air France iliyokuwa ikielekea jijini Paris, kwa ombi la Kinshasa ambalo limetaka arejeshwe DRC", chanzo cha polisi ambacho hakikutaka jina lake litajwe imeliambia shirika la habari la AFP.

Bwana Bakonga alikuwa akitafutwa na ofisi ya mashtaka tangu Aprili 16 kuhusiana na kesi ya ubadhirifu.

Waziri wa zamani wa Michezo chini ya utawala wa rais wa zamani Joseph Kabila, Bwana Bakonga alihudumu tangu Agosti 2019 kama waziri wa Elimu ya Msingi na Sekondari nchini DRC katika timu ya serikali iliyojiuzulu ya Rais Félix Tshisekedi.