DRC

Félix Tshisekedi aahidi kuchukuwa hatua kali dhidi ya magaidi mashariki mwa DRC

Rais w DRC, Félix-Antoine Tshisekedi Tshilombo akimkaribisha mwenzake Uhuru Kenyatta, Rais wa Kenya, katika ziara yake ya kiserikali ya saa 48 jijini Kinshasa.
Rais w DRC, Félix-Antoine Tshisekedi Tshilombo akimkaribisha mwenzake Uhuru Kenyatta, Rais wa Kenya, katika ziara yake ya kiserikali ya saa 48 jijini Kinshasa. © Présidence RDC / twitter.com

Rais wa DRC Félix-Antoine Tshisekedi ameapa kutokomeza uasi na machafuko katika mashariki mwa nchi hiyo katika siku za hivi karibuni.

Matangazo ya kibiashara

"Wanajeshi wa Kenya watawasili nchini DRC katika wiki zijazo kusaidia vikosi vyetu vya kijeshi ili kushambulia kwa njia bora zaidi kwa kutokomeza kabia tatizo hili la ugaidi na vurugu mashariki mwa nchi yetu", Rais Tchisekedi amtangaza leo Jumatano Aprili 21 .

Rais Felix Tshisekedi amesema hayo Jumatano hii mjini Kinshasa wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.

Kulingana na Rais Tshisekedi, mkutano wao umelenga hasa masuala ya usalama na uchumi. Mikataba kadhaa katika nyanja ya ulinzi na usalama kati ya mikataba mingine imesainiwa kati ya nchi hizo mbili.

Jeshi la Kenya kusaidia FARDC

Kama unavyojua, Kenya imekubali kwa hiari kuwa sehemu ya FIB, kikosi cha kuingilia kati kwa haraka, kilichoundwa na Umoja wa Mataifa kusaidia jeshi la FARDC mashariki mwa nchi yetu. Na katika wiki zijazo, wanajeshi wa Kenya watawasili DRC kusaidia vikosi vyetu vya kijeshi ili kushambulia kwa njia bora zaidi ili kukomesha tatizo hili la ugaidi na machafuko mashariki mwa nchi yetu.
Kwa hivyo, nachukua fursa hii kukosoa shutuma hizi zote za uwongo kwa madai kwamba hatusaidi au hatujishughulishi na hali ya Mashariki mwa DRC. Ninawaomba muelewe kwamba operesheni yetu itakuwa kubwa kali hadi kukomesha ghasia hizi mashariki mwa DRC.

Kwa upande wake, rais wa Kenya ametangaza hasa kufunguliwa kwa ubalozi mdogo mjini Goma na Lubumbashi kama sehemu ya kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.