ETHIOPIA

Ethiopia: Marekani yadai kuwa wanajeshi wa Eritrea bado wapo Tigray

Asmara, mji mkuu wa Eritrea.
Asmara, mji mkuu wa Eritrea. REUTERS/Thomas Mukoya

Bado hakuna ushahidi wa kuondolewa kwa wanajeshi wa Eritrea katika jimbo la Tigray, wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema, ikithibitisha habari kutoka Umoja wa Mataifa.

Matangazo ya kibiashara

Mwishoni mwa mwezi Machi, Waziri Mkuu wa Ethiopia kwa mara ya kwanza alikiri kuwepo kwa wanajeshi wa Asmara huko Tigray. Alitangaza kuwawanajeshi hao wameanza kuondoka katika jimbo hilo, lakini vyanzo kadhaa vinathibitisha kwamba bado wapo.

Kwa upande wa Marekani wanasema kuwa vikosi vya Eritrea bado viko katika jimbo hilo. Washington imetoa wito tena wa kuondoka kabisa kwa wanajeshi hao. Kuondoka kwa wanajeshi wa Eritrea katika imbo laTigray "ni muhimu katika kurejesha amani na usalama," amesema Ned Price, msemaji wa wizara ya mambo ya nje.

Soma pia: Wanajeshi wa Eritrea waanza kuondoka Tigray

Taarifa hii inathibitisha ile ya wiki iliyopita iliyotolewa na Mark Lowcock mbele ya Baraza la Usalama la Umpja wa Mataifa. Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu alibaini kwamba hakukuwa na ushahidi wa kuondoka kwa wanajeshi wa Eritrea katika jimbo la Tigray.