CHAD

Chad yamzika kiongozi wake wa muda mrefu Idriss Deby Itno

Jeneza la rais wa Chad Idriss Déby wakati wa mazishi yake ya kitaifa huko Ndjamena, Aprili 23, 2021.
Jeneza la rais wa Chad Idriss Déby wakati wa mazishi yake ya kitaifa huko Ndjamena, Aprili 23, 2021. AFP - CHRISTOPHE PETIT TESSON

Kiongozi wa muda mrefu wa Chad Idriss Deby aliyefariki dunia mapema wiki hii anazikwa leo Ijumaa. Viongozi mbalimbali duniani wamewasili katika mji mkuu wa Chad, Djamena ktoa heshima za za mwisho kwa rais huyo ambaye wpnzani wanasema aliitawala Chad kwa mkono wa chuma.

Matangazo ya kibiashara

Wakuu wa nchi kumi na moja ikiwa ni pamoja na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, rais wa DRC Félix Tshisekedi, rais wa Niger Mohamed Bazoum na Mkuu wa ser za mambo ya nje wa UlayaJ osep Borrell wako Ndjamena, mji mkuu wa Chad, kwa mazishi ya Rais Idriss Déby. Hata hivyo rais wa Congo Denis Sassou-Nguesso hatahudhuria mazishi ya kiongozi huyo akieleza sababu za kifamilia

Hafla hiyo imetanguliwa na ibada ya kidini kwenye msikiti mkuu mjini N'Djamena na mwili wa Deby unatarajiwa kusafirishwa kwa ndege ya kukodi na kuzikwa kwenye kijiji cha Amdjarass, mashariki ya nchi hiyo karibu na mpaka na Sudan, alikozaliwa.

Kifo cha Deby, aliyeiongoza Chad kwa zaidi ya miongo mitatu kilitangazwa na jeshi la nchi hiyo siku ya Jumatatu kutokana na kile kilichotajwa kuwa majereha aliyoyapata akiwa mstari wa mbele kwenye uwanja wa mapambano dhidi ya waasi.