UGANDA-DRC

Uganda yajibu madai ya DRC mbele ya ICJ

Mahakama ya Haki ya Kimataifa (ICJ) huko Hague, Agosti 27, 2018.
Mahakama ya Haki ya Kimataifa (ICJ) huko Hague, Agosti 27, 2018. REUTERS/Piroschka van de Wouw

Suala la kulipa fidia limekuwa limegubika mijadala inayoendelea tangu Jumanne katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki ya ICJ huko Hague.

Matangazo ya kibiashara

Mnamo mwaka 2005,  Mahakama hii ya Umoja wa Mataifa iliipata Uganda na hatia ya kuingilia maswala ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kuagizwa kulipa fidia kwa uharibifu uliofanywa wakati wa uvamizi wa jeshi la Uganda huko Ituri, hasa, kati ya mwaka 1998 na 2003. Kinshasa inadai Kampala zaidi ya dola bilioni 13.

Kwa upande wa Uganda inasema, madai ya DR Congo "hayana msingi", "hayaeleweki" na "yamepitwa na wakati". Kampala inasema Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeshindwa kutoa ushahidi kuhusiana na madai yake.

Uganda pia imekataa kulipia fidi kuhusiana na uharibifu uliofanywa kati ya mwaka wa 1998 na 2003, ikibaini kwamba nchi zote mbili zilihusika katika uharibifu huo, kama alivyiambia mahakama wakili mkuu wa Uganda, William Byaruhanga alivyoiambia: "Kwa kweli, kulikuwa na mizozo kadhaa iliyohusisha majeshi kutoka nchi tisa Angola, Burundi, Chad, DRC, Libya, Namibia, Rwanda, Sudan na Zimbabwe - na makundi 21 yenye silaha.