CHAD

Chad: Wanajeshi 12 na raia wauawa katika shambulio jipya la Boko Haram

Jenerali Mahamat Idriss Déby, rais wa Baraza la Jeshi la Mpito na mtoto wa hayati rais Idriss Déby Itno wakati wa mazishi ya baba yake Aprili 23, 2021.
Jenerali Mahamat Idriss Déby, rais wa Baraza la Jeshi la Mpito na mtoto wa hayati rais Idriss Déby Itno wakati wa mazishi ya baba yake Aprili 23, 2021. AFP - CHRISTOPHE PETIT TESSON

Shambulio jipya la Boko Haram limetokea katika Jimbo la Ziwa Chad, Jumanne hii, Aprili 27 asubuhi. Kundi la wanamgambo wa Kiislam wameshambulia kituo cha jeshi huko Litri katika Kaunti ya Kaya mwendo wa saa 11 asubuhi.

Matangazo ya kibiashara

Takriban wanajeshi 12 wa Chad na raia kadhaa wameuawa, wakati zaidi ya wapiganaji 40 wa Boko Haram walipoteza maisha, kulingana na ripoti ya muda iliyowasilishwa kwa RFI na gavana wa Jimbo la Ziwa Chad, Mahamat Fadoul Mackaye.

Mahamat Fadoul Mackaye amehakikisha kwamba "hali sasa inadhibitiwa". Vyanzo vya kijeshi kwene eneo la tukio vinaripoti wanajeshi 13 na wanajihadi 17 waliuawa wakati wa mapigano hayo.

Mahamat Idriss Déby alihutubia taifa

Wiki moja baada ya kuteuliwa kama kiongozi wa kamati ya kijeshi ya mpito, mtoto wa hayati Idriss Deby, Mahamat Idriss Deby Itno amewataka wananchi wake kuheshimu sheria na kujiepusha na vurugu ambazo zinaweza kuliweka hatari taifa la Chad.