ETHIOPIA

Marekani yashinikiza Ethiopia kuondoa wanajeshi wa Eritrea

Kulingana na vyanzo mbalimbali, wanajeshi wa Eitrea walitekeleza uakatili dhidi ya raia wa jimbo la Tigray kwa ushirikiano na wanajeshi wa Ethiopia, madai ambayo nchi hizo mbili zinakanusha.
Kulingana na vyanzo mbalimbali, wanajeshi wa Eitrea walitekeleza uakatili dhidi ya raia wa jimbo la Tigray kwa ushirikiano na wanajeshi wa Ethiopia, madai ambayo nchi hizo mbili zinakanusha. AFP - EDUARDO SOTERAS

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amemshinikiza Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed kuwaondoa "mara moja" wanajeshi wa Eritrea waliohusika katika mzozo katika jimbo la Tigray, wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema katika taarifa.

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa iliyoripoti mazungumzo ya simu kati ya waziri wa mambo ya nje wa Marekan na kiongozi wa Ethiopia, wizara ya mambo ya nje ya Marekani imebaini kwamba Antony Blinken amesema wanajeshi wa Eritrea walikuwa wakichangia maafa ya kibinadamu yanayoongezeka katika jimbo la Tigray.na walifanya ukiukaji wa haki za binadamu.

Antony Blinken pia "amesisitiza juuya umuhimu wa pande zote katika mzozo kumaliza mara moja uhasama," msemaji wa idara hiyo Ned Price amesema.

Wiki iliyopita Washington ilisema haikuona ushahidi wowote wa kuondoka kwa wanajeshi wa Eritrea katika jimbo la Tigray kama zilivyoahidi Ethiopia na Eritrea mapema mwezi huu.